Home Inside University DARUSO HISTORIA YA KUSISIMUA YA PROF. STEPHEN HAWKING.

HISTORIA YA KUSISIMUA YA PROF. STEPHEN HAWKING.

1188
0
SHARE

HISTORIA YA KUSISIMUA YA PROF. STEPHEN HAWKING.

Na:Goodluck Paul.

Stephen Hawking alikuwa mwingereza mwananadharia wa phizikia, mwanasayansi mashuhuriulimwenguni na mwandishi wa vitabu mbalimbali ambaye historia ya maisha yake ilianzaalipozaliwa Januari 8, mwaka 1942 hadi March 14 mwaka 2018 alipofariki dunia.

Kazi zake za kisayansi zinajumuisha ile aliyoshirikiana na Roger Penrose iliyohusu nadharia yanguvu ya kani ya uvutani na ile inayohusu uchomozaji wa miale ambayo pia ilipewa jina la Hawking.

Hawking alikuwa mwanasayansi wa kwanza kuweka nadharia ya asili ya ulimwengu ambayoilielezea nadharia za jumla na zile za asili ya vipimo vidogovidogo vya nishati.

Alijijizolea umaarufu mkubwa, heshima na tuzo nyingi ikiwemo Medani ya raisi ya uhuruiliyotolewa nchini Marekani. Alikuwa mwanachama wa taasisi mbalimbali Za kitaaluma. Mwaka2002, Hawking aliwekwa namba 25 miongoni mwa waingereza 100 wenye ushawishi mkubwa. Alifundisha kama professor wa hesabu katika chuo kikuu cha Cambrige nchini Uingerezakuanzia mwaka 1979 hadi 2009.

Alijipatia mafanikio makubwa ya kiuchumi kutokana na kazi yake ya uandishi ambayoilitambulika katika ulimwengu wa kitaaluma mathalani ile ya Popular Science ambayo ilijadilinadharia za asili ya ulimwengu na kile cha A brief history of time ambayo ilivunja rekodi yakuwa na mauzo bora ya nakala kwa takribani majuma 237 kwa mujibu wa Sunday times yaUingereza.

Hawking alipata ugonjwa uliojitengeneza taratibu uliojulikana kama Motor neuron disorder ambao ulifanya misuli yake ya mwili kudhoofu taratibu kwa miongo mingi kiasi hata cha kukosauwezo wa kuongea. Hata hivyo aliweza kuwasiliana na watu kwa kutumia kifaa maalumu cha kimawasiliano kilichofungwa mwilini mwake. Huu ndio ugonjwa uliopelekea mauti yake tarehe14 march mwaka 2014.

Hawking alizaliwa January 8 mwaka 1942 huko mjini Oxford Uingerezana baba yake Frank aliyezaliwa mwaka 1905 na mama yake Isobel ambaye alizaliwa mwaka 1913 na kufarikimwaka 2013. Hawking alizaliwa katika kumbukizi ya miaka 300 ya mwanasayansi mashuhuriulimwenguni, Galileo Galilei. Licha ya changamoto za kiuchumi za familia yake, wazazi waHawking wote walisoma chuo kikuu cha Oxford ambapo baba yake alisoma fani ya utabibu hukumama yake akisoma Falsafa, Siasa na Uchumi. Familia ya Hawking ilijiwekea utaratibu wa kilammoja kusoma vitabu.

Alianza safari yake ya kimasomo katika shule ya Byron House huko Highgate, London ambapoalilaumu sana kuhusu maendeleo yake baada ya kushindwa kujua kusoma. Baadae akiwa na umriwa miaka minane alihudhuria katika shule ya St Albans ambayo ilikuwa ya wasichana lakinivijana wadogo wa kiume waliruhusiwa kusoma, baadaye shule ya Radlett huko Hertfordshire. Kimsingi, familia yake ilithamini sana elimu. Mwaka 1958, kwa usaidizi wa mwalimu yake wahesabu, aliyeitwa Dikran Tahta, walitengeneza Computer iliyotokana na vifaa vya saa, simu zazamani na vifaa vingine vya aina hiyo.

Licha ya kujulikana kama “Einstein” akiwa shuleni, Hawking mwanzoni hakuwa na mafanikioya kitaaluma. Lakini kadiri muda ulivyozidi kwenda, alianza kuonesha kuhamasika katikamasomo ya sayansi huku akihamasishwa na mwalimu wake Tahta, alitamani  kusoma Hesabuhadi chuo kikuu. Hata hivyo baba yake alitaka asome fani ya utabibu, kwa kuwa hilihalikuwezekana, aliamua kusoma masomo ya Fizikia na Kemia.

Alianza elimu yake ya juu katika chuo kikuu cha Oxford mwaka 1959, akiwa na umri wa miaka17. Mwanzoni alighubikwa na upweke lakini baadaye katika mwaka wake wa pili na wa tatuchuoni, alijulikana na kujizolea umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake kitaaluma. Alipenda zaidi muziki na mambo yahusuyo Sayansi. Alikadiria kuwa alitumia saa 1000 kusomakatika miaka yake mitatu akiwa chuo kikuu cha Oxford. Alifaulu vizuri na kupata daraja la kwanza hivyo kutunukiwa shahada ya heshima katika Sayansi asilia.

Baada ya hapo alianza masomo ya shahada za juu katika chuo kikuu cha Cambridge mwaka1962, alijikita zaidi katika nadharia za jumla na zile zilizohusu asili ya ulimwengu. Wakati huougojwa wake ulizidi kumuathiri lakini taratibu huku akipoteza uwezo  wa kuongea. Lakini uleuchunguzi wa madaktari uliobaini kuwa alibakiza miaka miwili tuu ya kuishi ukadhihirika kuwahauna uhalisia. Wakati Hawking anaanza masomo ya shahada za juu, kulikuwa na mjadalamkubwa ulimwenguni kuhusu asili ya ulimwengu, hivyo akateua mada hii na kuiandikia tasnifuambayo ilipitishwa mwaka 1966.

Baada ya kufanya kazi nyingi ikiwemo uandishi wa machapisho ya kisayansi, alirejeaCambridge mwaka 1975 kwa ajili ya kazi na nafasi za juu za kitaaluma hasa katika Fizikia yaKani ya mvutano. Alizidi kutambulika zaidi katika ulimwengu wa kitaaluma. Mwaka 1975 alipata Medali ya heshima ya Eddington na medali ya dhahabu ya (Pius xi) na mwaka 1976 alipata tuzo Dannie Heineman, tuzo ya Maxwell na medali Hughes na mwaka 1977 aliteuliwakuwa Professor wa Fizikia ya kani ya uvutani na mwaka uliofuata alipata medali ya Albert Einstein kama udaktari wa heshima kutoka chuo kikuu cha Oxford. Baadaye mwaka 1979, aliteuliwa kuwa Professor wa hesabu katika chuo kikuu cha Cambridge.

Aliendelea kuandika kazi nyingi za kitaaluma ambazo zilikuwa msingi wa ujifunzaji wa sayansikote ulimwenguni.

Maisha yake ya ndoa yalianza baada ya kukomaa kwa mahusiano kati yake na binti Jane Wilde ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa dada yake ambaye walikutana kabla ya kuugua sana, nahatimaye walioana mwaka 1965. Katika mwaka wao wa kwanza wa ndoa, Jane aliishi London wakati akimalizia shahada yake ya awali, na Stephen na mkewe walisafiri kwenda Marekanimara kadhaa kuhudhuria mikutano mbalimbali ya Fizikia. Baadae Jane alianza masomo yake yaPHD na walibarikiwa kupata mtoto wa kwanza Robert ambaye alizaliwa mwaka 1967. Wa piliLucy mwaka 1970 na wa tatu Timothy mwaka 1979.

Licha ya kuwa aliugua sana, hakini Hawking alikuwa si aghalabu kuzungumzia ugonjwa wake. Mahusiano yake na mkewe Jane yalianza kuingia dosari kutokana na misimamo yake hasa ile yakidini kwani hakuamini katika dini jambo lililomkanganya mkewe ambaye alikuwa anaaminikatika ukristo.Hata hivyo mwishoni mwa miaka ya 1980, Hawking alianza mahusiano na mmojawa wauguzi wake Elaine Mason, na baadae alimuoa baada ya kuachana na mkewe mwaka 1995. Hata hivyo kabla ya hapo, mkewe Jane, tayari alikuwa kwenye mahusiano na mwimbajimwenzake wa kwaya Jonathan Hellyer.

Ugonjwa wa Hawking ulimfanya kupooza katika muda mwingi wa maisha yake. Hawking alifariki nyumbani kwake Cambridge, Uingereza asubuhi ya tarehe 14/03/2018 akiwa na umriwa miaka 76, safari yake ya mwisho ilisindikizwa na watu wengi kutoka pande mbalimbali zadunia wakiwemo wanasayansi, wanamuziki na wanasiasa mashuhuri.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here