Home Inside University DARUSO The Message from President Jeremiah

The Message from President Jeremiah

458
0
SHARE

Na

Jeremiah John Jilili

Mwananchi wa Shinyanga(v)

0762634301/0687548035

SERIKALI IWASAIDIE WAKULIMA WA PAMBA NCHINI

Ndugu Watanzania tunatambua fika kwamba asilimia kubwa ya Watanzania wengi wanajishughulisha na kilimo na ufugaji ,zaidi Wananchi wa Kanda ya Ziwa hujishughulisha na kilimo cha zao la biashara liitwalo Pamba.

Mimi ni Mwananchi wa halmashauri ya Shinyanga,tumekuwa na Changamoto kubwa kuhusiana na bei ya pamba,soko pamoja na ubora wa pamba tunayoizalisha

Hivyo basi kama mwananchi ambaye natokea Mkoa wa Shinyanga ambao pamba ni zao kuu la biashara nimekuwa shahidi wa kero hizi kwa mda mrefu sasa hivyo basi ninapenda kutumia fursa hii adhimu kuwaomba waheshimiwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwani najua vikao vinaendelea Dodoma kuwasaidia wakulima wa pamba Nchini kwa kuwasilisha kero zao kwa serikali ili zitafutiwe ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Ninaomba Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamuunge mkono Mbunge wa kishapu ndugu Suleman Nchambi kwa hoja yake binafsi na ya msingi aliyoiwailisha bungeni kujadili mustakabali mpana wa bei,soko na ubora wa zao la pamba nchini..

USHAURI WANGU KWA SERIKALI KUPITIA WIZARA ZA KILIMO NA VIWANDA KUHUSU MSTAKABALI WA BEI,SOKO NA UBORA WA ZAO LA PAMBA

1.Serikali iweke mkakati madhubuti wa kutumia Raslimali pamba katika kukuza uchumi wa taifa letu.Ni wakati sasa serikali kuwekeza katika tekonolojia ya kisasa na mbinu Mpya za kilimo cha pamba ikiwa ni pamoja upunguzaji wa uingizwaji wa bidhaa zitokanazo na zao hili la pamba kutoka nje ya Tanzania na Kuhamasisha watanzania Kutumia bidhaa za ndani zitozotokana na zao hili.Hii itasaidia kukuza uchumi na kutengeneza ajira kwa Watanzania wengi.

2.Serikali kupitia bodi ya pamba kuweka bei elekezi zinazorudisha gharama za kilimo cha zao hilo Kwani ni zao linalohitaji gharama kubwa katika uendeshaji wake,hivyo serikali iweke utaratibu maalum kwenye pamba kama ambavyo inafanya kwenye zao la korosho unaozuia walanguzi kujipangia bei zao na kuwakandamiza,kuwanyonya na kuwaumiza wakulima

3.kuwatafutia wakulima mbegu za kisasa,kutoa elimu ya kilimo cha kisasa na kufuatilia kwa ukaribu sera ya utoaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati ili kuongeza ufanisi wa kilimo cha zao hilo Kwani bado kuna Changamoto katika upatikanaji wa pembejeo hizo kwa wakati

Mwisho nikutakie kila la kheri mbunge wa kishapu Ndugu suleman Nchambi kwa kuiona hiyo kero inayotukumba sisi wananchi wa Shinyanga,Simiyu,Mwanza,Tabora na mikoa mingine katika kilimo cha pamba

Viva Tanzania

Viva Uzalendo@🇹🇿

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here