Home News Inside University The message from President Jeremiah 26/01/2018

The message from President Jeremiah 26/01/2018

206
0
SHARE

Na JILILI J JEREMIAH

Daruso-President

0762634301

TAARIFA KWA UMMA WA DARUSO

Ndugu zangu Wanadaruso nawasalimu kwa kauli mbiu ya Daruso “SOLIDARITY FOREVER” Ndugu zangu itakumbukwa Kuwa kuelekea siku kuu ya Christmas na Mwaka Mpya nilitoa taarifa kwa umma wa Daruso kama mrejesho wa Changamoto mbalimbali ambazo ziko hapa chuoni,Changamoto hizo nilizianisha kama:-

1.kuchelewa kuanza kufanya kazi kwa Cafteria ya Magufuli

2.kutokuwepo na huduma ya chakula kijitonyama-CoICT

3.Miundo mbinu ya barabara ya kuelekea kwenye hostel za Magufuli

4.kutokufunguliwa kwa Daruso Bar takribani mwaka wa tatu sasa

5.etc

Lakini pia kama serikali nilieleza fika Kuwa Changamoto hizi tumekuwa tukizifuatilia kwa ukaribu sana katika sehemu zinazohusika hapa chuoni, na tusingeweza pia kutoa mrejesho katika kila hatua tunayopitia katika kufuatilia hizi Changamoto na Ndio maana mlitupa dhamana ya kuwa viongozi wenu.

Ndugu zangu mtakumbuka pia Kuwa niliwaahidi ya kuwa mda mfupi mara baada ya mwaka Mpya kuanza Cafteria ya Magufuli na Kijitonyama zingeanza kufanya kazi na hii ni kutokana na majibu na ahadi ambazo kama viongozi wenu tulifuatilia na tukakubalina hivo na ndio maana tukapata ujasiri wa kulileta kwenu,sasa pamoja na Changamoto za kiafya ambazo zilipelekea kuchelewa kwa Cafteria ya Magufuli kufunguliwa ambazo tulizizungumza kwa pamoja kwenye kikao cha 06/01/2018 kwenye kikao tulichokaa katika hostel za Magufuli na tukakubaliana yafuatayo:-

1.baada ya hapo Changamoto hizo kama kuweka vifusi kwa ajili ya kufukia mashimo yaliyokaribu na Cafteria,Kuweka umeme pamoja na kuweka mfumo wa majitaka pale Cafteria zingetafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo ili Cafteria ianze kufanya kazi lakini Mpaka sasa hatua zilizochukuliwa hazilizishi na zinaonyesha wahusika bado hawajatoa kipaumbele katika eneo hili muhimu kwetu.

2.Cafteria ya kijitonyama ambayo haina tatizo lolote la kimiundo mbinu mpaka sasa ili bidi ianze haraka iwezekanavyo lakini cha ajabu mpaka sasa haijafunguliwa na ikumbukwe kwamba kwa sababu ya ukosefu wa chakula ndani ya Hostel za kijitonyama Wanafunzi wanalazimika kuvuka barabara kwenda kuchukua chakula nje ya hostel hizo kitu ambacho ni hatari kiusalama haswa wakati wa usiku Kwani Mpaka sasa wako wanafunzi wenzetu takribani watatu ambao wamepata ajali na kujeruhiwa wakati wa kuvuka barabara wakienda kutafuta chakula wakati wa usiku maeneo ya Kijitonyama.

3.Ni mwaka wa tatu sasa toka Daruso bar ifungwe huku ikiwa inaonekana Wanadaruso wanaihitaji kwa kiwango kikubwa sana na sasa imegeuka Kuwa mtaji wa sera ya kila mgombea wa Urais wa Daruso kuahidi kuirudisha Daruso Bar,Mara baada ya kuingia madarakani Mimi pamoja na serikali yangu tumefanya jitihada kubwa na za dhati kufuatilia hatima ya Daruso Bar tukiwa tunaamini itaepusha safari za nje ambazo hazina msingi kama huduma zilizokuwa zinatolewa Daruso Bar zitaanza kupatikana,

Lakini (as usual) kumekuwa na ukwamishaji ambao hauna tija na sasa hauvumiliki tena na kama PMU hii kazi imewashinda watupe sisi ndani ya mda mfupi tutapata muwekezaji.

My take

1.”Idara ambazo zimekuwa zinaongoza kwa urasimu hapa chuoni kama PMU zitambue kuwa kipaumbele cha kwanza hapa ni kutoa huduma na sio biashara wala maslahi binafsi kama ambavyo inaonekana sasa”

2.Kwa sababu mambo yote hayo niliyoyaorodhesha hapo juu ni ya msingi sana katika ustawi wa afya na taaluma zetu hapa chuoni,na kwa sababu Daruso tumejiridhisha bila mashaka Kuwa kuna baadhi ya Idara hapa chuoni kama ESTATES na PMU zimekuwa kero kubwa na chanzo cha kukwamisha mambo mengi katika uendeshaji wa serikali yetu na chuo kwa ujumla.

Kwanza ninawaomba tuwe kitu kimoja katika kusimamia yafuatayo

(i )Cafteria ya Magufuli pamoja na CoICT zianze kufanya kazi kabla ya ijumaa ya tarehe 2/2/2018

(ii)Tunataka Daruso Bar ifunguliwe kabla ya tarehe 16/2/2018

(iii) barabara ya kuelekea Magufuli itengenezwe kabla ya tarehe 16/2/2018

Kama kufikia ijumaa ya tarehe 2/2/2018 Cafteria ya Magufuli na Kijitonyama zitakuwa hazijafunguliwa,kama ambavyo kauli mbiu ya serikali yetu ya 2017/2018 inavyosema “UNITED WE STAND,DIVIDED WE FALL” itabidi kwa umoja wetu tukutane Magufuli Hostel saa 12 jioni ili tuweze kusikiliza kwa pamoja kutoka sehemu zinazohusika na kutatua hizo Changamoto tajwa hapo juu ili tuweze kujua ni sababu gani haswa kiasi cha kuendelea kuona wanafunzi wenzetu wanapata ajari kwa sababu ya kutafuta chakula na bado kinaonekana ni kitu cha kawaida kwa anayehusika na hili suala pengine tu kwa sababu hajapata Mtu anayemtaka yeye awekeze,

Kama watashindwa kujitokeza na kutupa majibu ya kuridhisha kuhusu hizo Changamoto zetu tutajadili kwa umoja wetu,ni wapi sehemu sahihi inaweza ikasikilizwa ili tuende tukaombe msaada wa Changamoto hizi kutatuliwa

(i)tunalazimika kuamini ni urasimu na matumizi mabaya ya ofisi yasiyozingatia kujali maslahi ya umma kwa sababu Kijitonyama hakuna Changamoto yoyote ya kimiundo mbinu na bado Kila siku hali ni ileile, je ni kweli muwekezaji kakosekana??

(ii)huwezi kutuaminisha Kuwa mpaka Leo muwekezaji wa Daruso Bar amekosekana ili Hali watu wengi wamekuja ofisi zetu za Daruso wakiomba kuwekeza katika eneo hilo na katika kufuatilia kwetu tuliahidiwa Kuwa Daruso Bar ingeanza kufanya kazi kabla ya 25/12/2017 lakini baada ya muda ahadi hiyo ikayeyuka ghafla

Naomba nitumie fursa hii tena kuziomba idara husika kama PMU na ESTATES kuweka pembeni maslahi binafsi na kupunguza urasimu (bureaucracy) ambao hauna tija katika kufanikisha mambo ya msingi kama haya ambayo yanaathiri kwa kiwango kikubwa sana afya na taaluma zetu.

Mwisho niwatakie uwajibikaji mwema katika shughuli zenu za kila siku bila kusahau kufuata kanuni,taratibu na sheria za chuo pamoja na Nchi kwa ujumla

“UNITED WE STAND,DIVIDED WE FALL”

#🇹🇿@JILILI -26/02/2018

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here