Home Inside University DARUSO KUELEKEA SIKU YA KUMBUKIZI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

KUELEKEA SIKU YA KUMBUKIZI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

197
0
SHARE

KUELEKEA SIKU YA KUMBUKIZI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Na :

JILILI JEREMIAH JOHN

RAIS-DARUSO (0762634301)

Ndugu zangu Watanzania naomba nitumie fursa tunapoelekea siku ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa wito kwa Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kuyaenzi Mapinduzi haya kwa vitendo na kwa wivu wa Hali ya juu sana Kwani Mapinduzi haya Ndio yameasisi tunu mhimu tulizonazo leo kama vile amani,furaha,upendo na mshikamano baina ya Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla lakini pia Mapinduzi haya yamekuwa ni Chachu kubwa ya Maendeleo,Uhuru na Kusalimika kwa Raslimali zilizopo ndani ya mipaka ya Nchi yetu kutoka mikononi mwa Wakoloni.

Mwisho nitoe wito kwetu sisi vijana kutafakari kwa dhati na Kuwa na uelewa mpana wa mambo na agenda mbalimbali za Kitaifa na zile zenye misingi ya kiitikadi ili kutopoteza dhana halisi ya uzalendo kwa taifa letu Kwani tunaamini yako mambo mengi ambayo bila kujali tofauti zetu zote tutakuwa na mtizamo mmoja kwa maslahi mapana ya Nchi yetu pendwa Tanzania 🇹🇿.

JUMBE ZANGU MBILI KWENU WA TANZANIA KWA UJUMLA NI:-

(1)

“TANZANIA MPYA NA HATIMA NJEMA YA NCHI YETU HAITAJENGWA NA RAIS AU VIONGOZI PEKE YAO BALI IKO MIKONONI MWETU PIA,HIVYO WATANZANIA TUCHUKUE HATUA SAHIHI SASA ”

(2)

Maandiko matakatifu katika waraka wa Yakobo yanasema”yafaa nini mtu akisema ana imani lakini hana matendo? “(Yakobo 2:14)

“Hivyo basi ni imani yangu kubwa kuwa kumbukizi ya Mapinduzi haya ya Zanzibar yatakuwa ni chachu ya kutafsiri imani,sera,falsafa na mambo mengine mengi mazuri katika Nchi yetu kwa vitendo kama ambavyo Yakobo mtumwa wa Mungu anatusihi na kutuelekeza katika ule waraka wake kwa watu wote ya kwamba imani bila matendo,imekufa

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Zanzibar@🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here