Home News Inside University News about the Students’ Accommodations

News about the Students’ Accommodations

959
0
SHARE

Na

Rais wa Daruso Ndugu Jeremiah John Jilili

0687548035

KUHUSU TAARIFA ZA MAJENGO MAPYA YA MAGUFULI

Daruso tumefuatilia kwa karibu zaidi kujiridhisha juu ya picha zilizosambazwa kama mipasuko ya mabweni (hostels)mpya yaliyojengwa na udhamini wa Rais wa Tanzania DK.John Pombe Joseph Magufuli katika chuo kikuu cha Dar es salaam.

Yale ni majengo ambayo yamejengwa ukiyaona unaweza ukadhani ni jengo moja Lakini ukweli yanasehemu ambayo yanatenganishwa(separation points) amabayo ndiyo iliyo pigwa picha kama mpasuko (cracks) baada ya ubao uliokuwa umewekwa pale kuondolewa,na kulifanyika kitu tunachokiita kuongeza ukubwa wa uwazi huo kwa njia ya ku “ZOOM ” na hivyo kuupotosha umma

Kamati imeundwa nadhani itatoa ripoti ya kitaalamu kuhusu Hilo Lakini kwa ujumla kutoka kwa meneja wa magufuli hostel,wahandisi wa chuo kikuu,wahandisi wa Project hio na sisi wenyewe kama viongozi wa Daruso ambao hatuwezi kukubali watu wetu wakae sehemu ambayo sio salama tumejiridhisha pasi na shaka Kuwa hakuna tishio la kiusalama kwa wakazi wa mabweni hayo kama ambavyo watu wanajaribu kutaka kuuaminisha umma.

Kama Daruso hatuwezi kamwe Kuwa sehemu ya kuunga mkono watu ambao wamekuwa wakipinga ujenzi wa hio project ya hostel hizi Kama mtaji wao wa kisiasa hostel hizi zinabeba watu 3840 ikiwa Ni idadi kubwa kuliko watu wanaokaa main Campus,Kwani wakati ambao sisi tumejengewa mabweni haya Ni Wajibu wetu kama jumuiya ya Chuo kikuu cha Dar es salaam Kama kweli sisi ni waungwana kushukuru kwa Ujenzi huo Kwani Mhe Rais Angeweza kujenga sehemu zingine Lakini akaamua kujenga kwetu na sio kila kitu Ni siasa Kwani kwa ujenzi huo Mhe Rais amegusa Maisha ya wanafunzi na wazazi kwa ujumla wake Kwani wazazi walitakiwa kuhakikisha watoto wao wanawatafutia sehemu za kukaa.

Mwisho nitoe rai kwa wana Daruso kufuata kanuni,taratibu,sheria na miongozo ya chuo kikuu cha Dar es salaam pale ambapo wamebaini kuna Mambo yanahitaji kutatuliwa Kwani sheria ziko wazi kuhusu nani Ana mamlaka ya kuzungumza juu ya mambo ya chuo na si kila mtu anaweza akazunhumza anachojisikia kwa niaba ya Taasisi hii.

Ukizingatia taasisi za Elimu Ni miongoni mwa taasisi zinazohitaji amani na utulivu (peace and tranquility) kwa Kiwango kikubwa kama mazingira rafiki kwa wanafunzi kupata Elimu Yao,hivyo Ni waombe ridhi wote walioshitushwa na taarifa hiyo.

Mungu Ibariki Africa,Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Daruso

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here